Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba
Kwa ufupi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya jiji hilo, Kiomoni Kibamba amesema idadi hiyo ya wanafunzi ni kubwa ikiwa ni sawa na kiwango cha wananfunzi wanaokuwa katika shule zingine kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.
Mwanza. Shule ya Msingi Buhongwa iliyopo katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza imeandikisha wanafunzi 500 wa darasa la kwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya jiji hilo, Kiomoni Kibamba amesema idadi hiyo ya wanafunzi ni kubwa ikiwa ni sawa na kiwango cha wananfunzi wanaokuwa katika shule zingine kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.
Amesema kwa ujumla jiji zima la Mwanza limeandikisha wanafunzi 16,000 na bado linafanya hivyo, licha ya kukabiliwa na hali ngumu ya miundombinu ya kuwahifadhi wanafunzi hao na ya ufundishaji.
Kibamba ametoa taarifa hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mery Tesha alipokutana na madiwani, watendaji wa kata na mitaa wa jiji kuwapa maelezo ya ziara aliyoifanya mwishoni mwa mwaka jana.
Awali, Diwani wa Butimba, John Pambalu amehoji kwa nini mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa shule za Serikali bado ni mabovu licha ya halmashauri kutamba kuwa imeongeza makusanyo.
Hata hivyo, Kibamba amesema ukusanyaji huo wa mapato bado haujaweza kukabiliana na mahitaji yaliyopo.
“Hadi sasa Shule ya Msingi Buhongwa darasa la kwanza pekee lina wanafunzi 500, darasa la pili wanafunzi 400 sawa na uwezo wa kawaid
0 Comments