JKCI NDIO KIMBILIO


 Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima mapigo ya moyo Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma Mariam aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo. JKCI ilishiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya  bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri jumla ya wagonjwa 408 walihudumiwa katika banda hilo.

Mtaalamu wa Afya na Mazoezi ya viungo kutoka Chama Cha Wafanya Mazoezi Tanzania Waziri Ndonde   akiwaelekeza wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umuhimu wa kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua   kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo  kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.

 Mtaalamu wa Dawa na Tiba kutoka Hospitali ya SANITAS Dk. Sajjad Fazel akiwafundisha wananchi  waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya vyakula bora wanavyotakiwa kula ili waepukane na magonjwa yasiyoambukiza. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua   kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.

 Mratibu wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watu wazima na magonjwa ya saratani kutoka Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Sara Maongezi akiwafundisha wananchi  waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina za saratani na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara. Hivi karibuni Wizara hiyo ilizindua   kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bure kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.

Twaha Dofa (aliyeshika karatasi) akitoka kupima magonjwa ya moyo katika banda la  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya  bila malipo kwa siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto na kufanyika  katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.

0 Comments