JESHI la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Sanani iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Anitha Abel (21) kwa tuhuma za kukutwa na kete 15 za unga unaodhaniwa ni dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, alisema tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu saa 12 jioni katika Mtaa wa Mshikamano katika Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.
Alidai kuwa mtuhumiwa alikutwa katika harakati za kuuzia wateja dawa hizo, alipoona askari alikimbilia chooni, lakini alikamatwa.
Alisema Anitha anaendelea kuhojiwa na huenda akataja kundi la watu anaojihusisha nao.
0 Comments