Kwa ufupi
Taarifa kutoka TCU kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.
Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU)
imetoa ufafanuzi kuhusu wanafunzi 8,357 waliotajwa kuwa hawana sifa stahiki za kuendelea na elimu ya juu na kudai kwamba kulikuwa na dosari katika taarifa zao.
Taarifa kutoka TCU kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.
Taarifa hiyo imesema wanafunzi wote walioorodhesha katika taarifa iliyotolotewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao ya kawaida.
“TCU inapenda kuuarifu umma kuwa ,uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa kifungu 5(1)(b)c) cha Sheria ya Vyuo vikuu Sura ya 346 YA Sheria za Tanzania,’’imesema taarifa hiyo.
0 Comments