TUCTA YAWATETEA WADAIWA WA BODI YA MIKOPO (HESLB)

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokwa 

Kwa ufupi

Akizungumza leo (Jumanne) Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokwa amesema wafanyakazi hao waliingia mkataba na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ya kukatwa asilimia nane.

By Mwananchi

Dar es Salaam.  Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limetoa siku 14 kwa Serikali kuwarejeshea wafanyakazi fedha za mikopo ya elimu ya juu wanazokatwa kimakosa vinginevyo watafanya uamuzi mgumu

Akizungumza leo (Jumanne) Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokwa amesema wafanyakazi hao waliingia mkataba na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ya kukatwa asilimia nane.

Amesema baada ya sheria mpya iliyopitishwa Agosti 2016 imebadilisha na sasa wanakatwa asilimia 15 bila kujali walikopa lini mikopo hiyo.

"Tunataka waliokopa kabla ya kupitishwa sheria hii waendelee kukatwa asilimia nane na siyo asilimia 15 wanayokatwa" amesema.

0 Comments