Kwa ufupi
Battista mkazi wa Wisconsin, Marekani alisema aliamua kutoa figo hiyo ili aokoe maisha ya mtoto huyo baada ya kusikia jinsi anavyoteseka kutokana na figo hiyo kufeli.
Wisconsin. Mwalimu wa Chekechea, Beth Battista ameamua kujitolea figo yake moja ili kuokoa maisha ya mwanafunzi wake, Lyla Carreyn mwenye umri wa miaka mitano.
Battista mkazi wa Wisconsin, Marekani alisema aliamua kutoa figo hiyo ili aokoe maisha ya mtoto huyo baada ya kusikia jinsi anavyoteseka kutokana na figo hiyo kufeli.
Battista ameliambia gazeti la Insider la nchini humo kwamba hakusita kutoa figo yake baada tu ya kusikia jitihada za Lyla za kutafuta figo kwa muda mrefu.
Mwalimu huyo, ambae pia ni mama wa watoto wawili, amesema alisikia juu ya hali ya Lyla baada ya mama yake kuweka taarifa za mwanawe katika mtandao wa Facebook.
Mwaka mmoja uliopita, Lyla alipatikana na tatizo la figo ambapo alitakiwa kusafishwa damu kwa saa kumi na mbili kwa siku.
0 Comments