Uongozi wa Shule ya Msingi Maweni ukimtembeza mgeni rasmi kuangalia maeneo ya shule hiyo na changamoto zake.
Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akimuongoza Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita kuzungukia majengo ya shule hiyo kujionea changamoto zake akishirikiana na Mkuu wa shule hiyo,Zuhura Mwaliko.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam akiangalia dampo linalotumiwa na shule hiyo kutupia na kuchomea moto uchafu jinsi lilivyo.
Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akimuonyesha Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (katikati) eneo ambalo limewekwa kwa ajili ya kujengwa madarasa endapo fedha zitapatikana
Mkuu wa Shule ya Maweni,Zuhura Mwaliko akieleza jambo kwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita.
Mojawapo la darasa ambalo halijakamilika katika shule hiyo
Wakinamama waliojitokeza katika mkutano huo wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa madarasa ya shule ya maweni.
Wakinababa waliojitokeza katika mkutano huo wa harambee
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maweni wakiimba wimbo wa shule hiyo kabla ya mkutano kuanza.
Meya wa jiji la Dar es salaam akiwa na mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maweni akisoma Risala iliyoandaliwa na wanafunzi wa hapo
Wanafunzi walioshiriki katika mkutano huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo,Kabega Ally akizungumza katika mkutano huo..
Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akizungumza katika mkutano huo wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa shule hiyo. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maweni,Denis Edifonce akisoma risala iliyobeba ujumbe wa changamoto iliyonayo shule hiyo mbele ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Zuhura Mwaliko.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche akimtunza mwanafunzi aliyekuwa akicheza nyimbo za asili katika mkutano huo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko na Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akimpatia hela kijana Denis Edifonce aliyesoma risala iliyoandaliwa na shule hiyo ambayo ilikuwa na ujumbe mzito uliomgusa meya huyo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko na Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwitaakisisitiza jambo kwa viongozi walioko meza kuu kuhusu maendeleo ya kata ya Mji Mwema.PICHA NA ELISA SHUNDA
Mkazi wa Mtaa wa Maweni,Rehema Kitunda akizungumza kwa niaba ya wakinana mama wenzake na kuchangia ujenzi huo.
Mkazi wa Mtaa wa Maweni,Daudi Mwasambile
akizungumza kwa niaba ya wakinana mama wenzake na kuchangia ujenzi huo.
Burudani za ngoma za asili zikiendelea katika mkutano huo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwapongeza vijana wa ngoma za asili walionesha uwezo wao na kuwapa moyo wa kuzidi kujituma kutokana na vipaji walivyoonesha na kuwapa nafasi ya kufika ofisini kwake ili azungumze nao aone jinsi gani anaweza kuwasaidia ili wafike katika malengo yao waliyoyakusudia katika tasnia ya sanaa ya muziki.PICHA NA ELISA SHUNDA
Na Mwandishi Wetu,Dar es salaam.
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kuchangia mifuko 100 ya Simenti pamoja na Mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Maweni iliyopo Kata ya Mjimwema wilayani Kigamboni.
Shule hiyo ambayo inaupungufu mkubwa wa madarasa pamoja na uzio wa shule , inajumla ya wanafunzi 1300 ikiwemo na wale wenye ulemavu.
Akizungumza katika hafla hiyo ya chagizo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, Meya Isaya alisema kwamba hatua hiyo ni kwa jili ya kuzisaidia shule ambazo zinaupugufu wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi wasome katika mazingira salama.
Alisema kwamba wakati alipokuwa akiwania nafasi ya Udiwani Kwenye kata yake ya Vijibweni , na kisha kupata nafasi ya kuwa Meya wa jiji, moja ya vipaumbele vyake ilikuwa ni kuzisaidia shule ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa. “ Niseme tu kwamba jiji hili ambalo linarasilimali nyingi halafu wanafunzi wanakaa chini, sio jambo zuri, lazima watu ambao tumechaguliwa na wananchi ambao ndio wenye watoto wanasoma hapa, tutimize majukumu yetu” alisema Meya Isaya.
“ Kama kwenye Kata yako unaona kabisa wanafunzi wanakaa chini na wewe diwani upo, basi ujue huna sifa ya kuwa diwani na wananchi watakuwa na haki ya kukuondoa madarakani kwenye uchaguzi ujao.
Alifafanua kwamba” jambo la uchagiaji wa kusaidia wanafunzi wasikae chini sio la kisiasa bali ni katika sehemu ya kuwasaidia wananchi hivyo kuwataka wananchi kuondoa dhana ya kisiasa.
“ Hapa leo hii tukijenga madarasa kila motto anasoma akiwa amekaa kwenye madarasa mazuri, madawati ya kutosha, lakini watoto hao sio wa chadema, sio wa CCM wala CUF bali ni wananchi wote, nawaombeni sana kwenye suala la elimu tusilihusihwe na mambo ya siasa” alisema Meya Isaya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema, Selestine Maufi pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Isaya kwa kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule hiyo.
Hata hivyo Diwani huyo aliahidi kuchangia matofali 500 ,madawati 60 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa .
Hata hivyo awali akisoma lisara kwa mgeni rasmi iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo, Mwalimu Selemani alisema kwamba shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba kadhaa vya madarasa ambapo vilivyopo havikidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo.
Alifafanua kwamba kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wananfunzi wenye ulemavu wamelazimika kusomea kwenye chumba cha darasa kimoja jambo ambalo linawapa shida walimu kwenye ufundishaji.
0 Comments