Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF),Juliana Busasi (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maandalizi ya Kampeni ya kuboresha Afya Wanawake na Watoto ijulikanayo kama Nuru ya Afya inayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Jijini Dar es Salaam.
Shirika la Afya na Elimu ya Tiba-TAHMEF linatarajia kuendelea na Kampeni yake ya kuboresha Afya ya Wanawake na Watoto ili kuboresha Afya Bora na Ustawi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika hilo,Juliana Busasi amesema TAHMEF inatarajia kufanya shughuli maalum yakuchangia Mfumo wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto siku ya Jumamosi Machi 04,2017.
Amesema shughuli hiyo italenga mambo mawili ambayo ni Kuwekeza Bima za Afya ya Mama na Mtoto ikiwa kuchangia pesa,Kuwasaidia Bima ya Mwaka mmoja kukaa katika Mfumo na kuwekeza.
Pia kuboresha Mazingira katika Hospitali na kuchangia vifaa katika hospitali za Serikali.
Kwa upande wao Wanachama wa Shirika hilo,Kenneth Munanu na Consolata Msambichaka wamesema vijiji vingi hapa nchini vina uhitaji wa Bima ya Afya.
Pia wamewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia shughuli hiyo ili kufanikisha Kampeni hiyo ya Nuru ya Afya
0 Comments