KAIMU Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dk Bernard Achiula amesema Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inapaswa kuyajua masuala yadiplomasia kwa kuwa ni msingi wa uchumi.
Dk Achiula alisema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi vyeti kwa wahitimu 15 waliohudhuria mafunzo kuhusu Itifaki na Mahusiano ya Umma, yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam. Alisema umefika wakati taifa likatambua zaidi umuhimu wa TMA ili kunapotokea ukame, liweze kujiandaa na kuweka mikakati imara mapema ili kusitokee njaa.
“Ni muhimu kujua hali ya hewa ili tuweze kujipanga vizuri maana bila kilimo mahiri, siasa yetu ya viwanda haitaweza kukamilika,” alisema. Alisema watalii wanapaswa kufahamu hali ya hewa itakuwaje kabla ya kufanya utalii popote wanapokwenda nchini. Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema mafunzo waliyoyapata yameongeza kwa sehemu kubwa umuhimu wa shughuli wanazozifanya kwa kuwa wanapokusanya taarifa huzisambaza duniani kote. “TMA ina wajibu mkubwa wa kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa jamii, hivyo kupitia mafunzo haya washiriki wameongeza ujuzi ikiwemo lugha rahisi na ya kueleweka
0 Comments