MAENDELEO YA AFRIKA YANAWATEGEMEA VIJANA


Naibu Waziri wa Afya Wanawake Jinsia na Watoto , Dk Hamisi Kigangwala akifungua Kongamano la Vijana barani afrika juu ya Maendeleo barani Afrika.

Washiriki wa Kongamano hilo Vijana kutoka nchi Mbalimbali wakifatilia Hotuba ya Dk Kigwangala


Vijana barani Afrika wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kueleta Maendeleo hili kufikia malengo hasa katika kipindi hiki cha mapinduzi ya Teknolijia na Viwanda.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya Wanawake Jinsia na Watoto, Dk .Hamisi Kigwangalla alipokuwa akifungua kongamano la Vijana barani Afrika lililoandaliwa na Tasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais Kigwangala amesema kuwa mara zote vijana wanapokusanyika na kujadili maendeleo ya bara la Afrika ni muhimu sana kwani leo vijana ndio wadau wakubwa katika swala zima la maendeleo ya bara lao .

“Inaeleweka kabisa ukuaji wa bara la Afrika unategemea vijana ndio maana ajenda ya 2063 inahusisha ubunifu , Nishati , utamaduni na swala zima la siasa safi kama serikali tunawahimiza vijana kujitambua na kuwawezesha kufikia malengo hili kuweza kupambana na vikwazo vinavyo wakabili” amesema Kigwangala.

Ameongeza kuwa vijana wanatakiwa kutambua vikwazo vinavyo wakabili kama fursa ya kujipatia maendeleo kwa kutatua vikwazo hivyo kwa ajili ya maendeleo ya vijana wa kesho.

Amesema mjadala wa leo sio tu kwa ajili ya Vijana bali ni kwa ajili ya maendeleo ya bara la Afrika kwa kuwa na sera zitakazowawezesha vijana.

Rasi wa Vijana Barani Afrika , Francine Muyumba akizungumza na Vijana mbalimbali kutoka nchi mbalimbali ambao walishiriki kongamno hilo la Vijana.

Washiriki wa Kongamano wakisikilza kwa makini.

Mmoja wa Vijana kutoka nchini Nigeria, Arinze Obiezue akitoa neno la shukrani kwa naiba ya washiriki wa kongamano hilo.

Viongozi wa meza kuu wakiongoza na Naibu Waziri wa Afya , Dk Hasmisi Kigwangalla wakisikila maneno ya shukrani kutoka kwa kijana.

Picha ya pamoja ya Naibu Waziri na Washiriki wa Kongamano hilo

0 Comments