MJADALA WA VIJANA


Meneja Miradi wa Tamasha la Vijana, Churchill Shakim akiongoza mjadala wa kuichambua agenda ya vijana kuhusu bajeti kwenye nyanja mbalimbali ili serikali kuweza kufanikisha malengo hayo kwa vijana. (Picha zote na Geofrey Adroph)

  Mkurugenzi mtendaji wa Africa Youth Trust(AYT), Nahashon Gulali akizungumza na vijana waliokutana kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu bajeti hasa kwenye vipaumbele vya vijana kwenye bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma.



  Katibu Mtendaji wa TYVA na mratibu wa mtandao wa asasi za Vijana Tanzania, Ndugu Saddam Khalfan  akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa wakati wa kujadali na kufanyia uchambuzi bajeti hasa kwa kwenye mfuko wa vijana kwa mwaka 2017/18 uliofanyika katika ukumbi wa Wanyama jijini Dar es Salaam leo.

  Msimamizi wa Mradi kutoka AYT akiwasilisha kuhusu umuhimu wa vijana katika mpango wa bajeti ili kuweza kuinuka kiuchumi pamoja na kutolea ufafanuzi kuhusu taasisi ya AYT pamoja namradi wa Youth Action for Development effectiveness(YADE)  kwa vijana waliokutana ili kujadili vipaumbele vya vijana kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 kwenye mkutano uliofanyika katika hoteli ya Wanyama jijini Dar leo.

Baadhi ya vijana wakichangia mada wakati wa kuichambua agenda ya vijana iliyoandaliwa kuhusu mikakati ya bajeti kwa vijana kwenye mkutano uliowakutanisha vijana kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu bajeti hasa kwenye vipaumbele vya vijana 

Baadhi ya magroup ya vijana wakijadiliana kuhusu changamoto pamoja nakuja suluhisho kwenye masuala ya msingi ya vijana hasa kuwezeshwa kiuchumi kupitia bajeti ya mwaka  2017/18.

Mkutano ukiendelea

0 Comments