Mwakilisi wa UNICEF, Maniza Zaman akizungumza na Wahariri kwenye mkutano maalumu unaofanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro
Kwa ufupi
Hayo yamesemwa leo mjini hapa na mwakilishi wa shirika linalohudumia watoto duniani, (UNICEF), Maniza Zaman kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika mjini Moshi.
Moshi. Jumla ya watoto 269 wenye umri chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku nchini. Pia wajawazito 556 hufariki dunia pia kutokana na matatizo ya uzazi.
Hayo yamesemwa leo mjini hapa na mwakilishi wa shirika linalohudumia watoto duniani, (UNICEF), Maniza Zaman kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika mjini Moshi.
Zaman amesema kwa mujibu wa utafiti walioufanya, kwa upande wa elimu, asilimia 39 tu ya watoto wa kike na kiume ndiyo wanaohitimu elimu ya sekondari nchini kila mwaka.
"Wako wapi watoto wengine, kama nchi kuna kazi ya kufanya ili kuhakikisha watoto wetu wanapata mahitaji yao ya msingi, ikiwamo elimu na huduma bora za afya ili kuepusha vifo kwa watoto," amesema Zaman.
0 Comments