MJIMBAJI MDOGO AJENGA MADARASA, OFISI YA WALIMU

Kwa ufupi

Kibusu, mkazi wa Kitongoji cha Itumbi, Kata ya Matundasi wilayani hapa, alisema aliamua kuchukua hatua hiyo ili kuboresha kiwango cha elimu kijijini kwao. Shule ya Itumbi ilianzishwa mwaka 2002, ina wanafunzi 663 lakini miundombinu yake ilikuwa mibovu jambo lililo sababisha wanafunzi kujisaidia vichakani kwa zaidi ya miaka 15.

Chunya. Mchimbaji mdogo wa dhahabu, Edson Kibusu ameonyesha mfano baada ya kukarabati madarasa mawili, ofisi ya walimu na kujenga choo chenye matundu 18 katika Shule ya Msingi Itumbi.

Kibusu, mkazi wa Kitongoji cha Itumbi, Kata ya Matundasi wilayani hapa, alisema aliamua kuchukua hatua hiyo ili kuboresha kiwango cha elimu kijijini kwao. Shule ya Itumbi ilianzishwa mwaka 2002, ina wanafunzi 663 lakini miundombinu yake ilikuwa mibovu jambo lililo sababisha wanafunzi kujisaidia vichakani kwa zaidi ya miaka 15.

Akizungumza mjini hapa juzi, Kibusu alisema ameguswa zaidi na kitendo cha wanafunzi kusomea madarasa yaliyojaa vumbi, kujisadia vichakani huku walimu wakikaa katika ofisi mbovu.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Aporinary Michael alisema kitongoji hicho kina wakazi wengi wenye fedha lakini hawana moyo wa kujitolea.

Alisema alianza kazi shuleni hapo Machi mwaka jana na alihamasisha wazazi kuboresha miundombinu, lakini hawakuonyesha utayari.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa alimpongeza Kibusu kwa moyo aliouonyesha na kuwataka wadau wengine kumuunga mkono kusaidia taasisi zenye uhitaji kama huo.

“Ni mtu wa ajabu sana amefanya maajabu ya kipekee katika kitongoji hiki, nyie wenyewe mmeona muonekano wa shule umebadilika lakini na wengine muige kupitia yeye ili tuweze kusukuma gurudumu hili kwa pamoja,’’alisema Madusa.

0 Comments