PLATINUM YAICHIMBIA KISIMA SHULE YA MSINGI UHURU

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizindua kisima

Kwa ufupi

Ofisa rasilImali watu wa Platinum, Ladislaus Mwongerezi, kwa niaba ya Mkurugezi Mkuu alisema msaada huo ni kwa ajili kutatua changamoto ya maji inayoikabili shule hiyo pia kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano katika utoaji wa elimu.

Dar es Salaam. Taasisi ya Mikopo ya Platinum imetoa msaada wa ujenzi wa kisima cha maji chenye thamani ya Sh 8 milioni kwa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko iliyopo jijini hapa.

Ofisa rasilImali watu wa Platinum, Ladislaus Mwongerezi, kwa niaba ya Mkurugezi Mkuu alisema msaada huo ni kwa ajili kutatua changamoto ya maji inayoikabili shule hiyo pia kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano katika utoaji wa elimu.

"Platinum tuliitembelea shule hii  kwa ajili ya kutafuta biashara, kuzungumza na waalimu ili tuweze kuwakopesha fedha, wakati tukiwa katika mazingira haya tulibaini changamoto ya maji tukaona tusiishie kufanya biashara tu bali na kuangalia ustawi wa watanzania wenzetu," Mwongerezi

0 Comments