Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akikabidhi zawadi kwa mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tewe iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na ya sita kimkoa
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe wakisomewa namba na wanafunzi wa shule ya awali kabuku nje
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wakisikiliza mwanafunzi alipokuwa akielezea tense za somo la kiingereza
wanafunzi wa shule ya sekondari kabuku akielezea mifumo ya kibaiolojia Kwa viongozi
Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza wakati wa Hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe wakatikati na Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe wa mwisho kulia na kaimu afisa Elimu Msingi Bw Fikeni senzige wakikagua gwaride la wanafunzi wa kabuku.
mwalimu na wanafunzi wkisherehesha Hafla hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepongeza na kutoa zawadi kwa shule kumi za Msingi na moja Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne mwaka 2016. Zawadi hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la elimu yaliyofanyika kiwilaya Wilayani Handeni kwenye shule ya Msingi Kabuku nje.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Mh. Godwin Gondwe aliwapongeza walimu na wadau wengine wa elimu kwa kazi nzuri wanazofanya na wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
“elimu ni ufunguo wa maisha na kwamba Handeni hakuna mtoto mjinga, wazazi na walezi himizeni watoto kutumia fursa ya Elimu bure inayotolewa na Raisi wa Tanzania” Alisema.
Aidha ameeleza kuwa atahakikisha fedha zinazohusu madai ya walimu zinapofika Halmashauri zinawafikia walengwa kwa wakati uliopangwa. Aliwataka wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.
Wakati huohuo amepiga marufuku watoto walio na umri wa kuwepo shuleni kuacha kuchunga mifugo hasa kwa siku za shule baada ya kubainika watoto wengi wa jamii ya wafugaji wanatumiwa kuchunga mifugo badala ya kwenda shule.
Amewaonya wazazi na jamii ya wafugaji ambao wanakwamisha watoto kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu na kwamba sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume. Amewaeleza pia wazazi ambao wanawatoto waliovuka umri wa kwenda shule kupelekwa kwa utaratibu wa MEMKWA.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe ,amesema kuwa kukosekana kwa chakula cha kutosha shuleni,utoro uliokithiri kwa baadhi ya wanafunzi,kutokuwajibika kwa baadhi ya walimu na wazazi pamoja na upungufu wa walimu kunasababisha kwa kiwango kikubwa kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi.
Ameagiza shule ambazo mpaka sasa ambazo hazina chakula kuhakikisha wanawapa wanafunzi chakula. Aliwataka pia kusimamia mazao ya mihogo waliyopanda ili mazao hayo yaweze kusaidia upatikanaji wa chakula shuleni na kuongeza kiwango cha uelewa kwa wanafunzi.
Ametoa mwezi mmoja hadi kufikia 4/5/2016 kwa Maafisa watendaji Kata, Vijiji, walimu wakuu, wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kuhakikisha kuwa watoto wanapata chakula cha mchana shuleni.
Shule za Msingi zilizopata zawadi na pongezi ni Tewe iliyokuwa ya sita kimkoa na kuzawadiwa Tsh. 200,000/=., Chang’ombe Tsh. 150,000/=, Mkumba Tsh 100,000/=, Mzundu Tsh. 82,000/=, Kwaragulu , Mbwewe, Kwamdani, Kwedikwazu Magharibi, Kwedikwazu Mashariki na chogo ambazo zote zilipata Tsh 78,000/=. Mazingara sekondari imepata zawadi Tsh.100000/=.
0 Comments