Pongezi ya kujitolea toka Elimu Afrika anapewa kijana Tisekwa Gamungu kwa kazi iliyotukuta yakiutu, yakizalendo na Upendo wa kimungu kabisa.
Ni watoto wachache wanaweza kuokoka kwenye janga la kuzama maji na kuchua hatua ya kuwaokoa wengine, wewe ni kijana bora ambaye taifa lapaswa kuwekeza kwako kwakuwa utaenda kuwa hazina ya taifa. Kwa ufupi Tisekwa alielezea mkasa uliowapata wakiwa wanatoka shuleni alisema;
"Naitwa Tisekwa Gamungu nipo darasa la Tano na nina miaka 16. Ilikuwa jumatatu tumetoka shuleni na wenzangu, tulifika sehemu ya kupanda Boti tulifanikiwa kupanda boti na wenzangu lakini tulivyofika katikati boti zetu zilizama ikabidi niogelee na wenzangu ili kuweza kutoka nchi kavu lakini wenzangu wengine walishindwa. Hivyo ilinibidi niingi kuwaokoa wenzangu kwani moyo ulikuwa unaniuma kuwaacha wenzangu wazame wakati nina uwezo wa kuwasaidia. Nilifanikiwa kuwaokoa wenzangu 9. Wakati naendelea kuwaokoa, wenzangu 3 walichoka sana kwaiyo walizama. Nikajitahidi kuwatafuta lakini sikuwaona."
Kwa niaba ya Elimu Afrika nisema.
Shukrani kwa kujitolea kuokoa wenzako, umetoa elimu kwa vitendo , umethibitisha Uzalendo, Utayari na umefuzu thamani ya kuwa Tunu/Urithi wa Afrika.
Asante sana
Mr Daniel
Tufuatilie kupitia, Instagram: @elimuafrika, Facebook: Elimu Afrika, Twitter: @ElimuAfrika na YouTube: Elimu Afrika
#SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments