Dar es Salaam. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Lazaro Mbise (23) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na bastola aina ya LUGER cz100 pamoja na risasi 13 na fedha kiasi cha sh 800,000/= ambayo alimwibia baba yake, kama Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alivyothibitisha.
Nadhani ni wakati muafaka sasa upekuzi wa kina ukawa unafanywa kwenye vyuo na vyuo vikuu, ili kubaini kama kuna wengine wanaiba silaha mbalimbali au kukodisha kwa nia ovu.
Wanafunzi hasa wa vyuo na vyuo vikuu wanaweza kushirikiana na wahalifu kuhifadhi silaha hasa bastola kwa ujira mdogo toka kwa wahalifu, hatahivyo wanafunzi wameaminiwa nchi hii kwa kiwango ambacho wanahisi hawawezi kutiliwa shaka na MTU wala chombo chochote, hivyo pekuzi za kushtukiza zapaswa kufanyika Vyuoni na Vyuo Vikuu.
"Ualifu haujali umri wala hadhi, ni tabia"
Elimu Afrika
0 Comments