Fatma Jabir
Mwanafunzi atoweka , aliaga anakwenda kwa rafiki yake tangu mwanzoni mwa mwezi huu lakini hadi sasa hajarudi nyumbani.
Tanga. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Kange jijini hapa, Fatma Jabir (15) ametoweka kwa wiki mbili sasa huku jitihada za kumpata zikishindwa kuzaa matunda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema mwanafunzi huyoalitoweka nyumbani tangu Mei 6 mwaka huu na hadi sasa hajapatikana.
Mama wa mwanafunzi huyo, Swahiba Hashim (39) amesema kuwa mwanaye aliondoka nyumbani Jumamosi na kuaga kuwa anaenda kwa rafiki yake wa kike anayeishi Kichangani.
Swahiba ambaye ni mfanyabiashara ya duka amesema aliporejea nyumbani jioni kutoka kwenye mizunguko yake mwanaye hakuwa amerudi.
"Nikaenda kituo cha polisi kutoa taarifa nikapewa saa 24 za kusubiri ilipofika Jumatatu nikaenda tena kuwaambia kwamba hajarudi ndipo akakamatwa rafiki yake ambaye alipofikishwa kituoni licha ya kupigwa sana lakini alidai kwamba hajui aliko,"amesema.
Mama huyo amesema jitihada za kumpata zimeshindikana kwa kuwa ameshawasiliana na ndugu zake walioko mikoa mbalimbali ambao wamesema hajafika kwao na hata shuleni hajaonekana.
"Nisadieni jamani nimuone mwanangu kwani sijui kama ameuawa au yuko wapi nataka nimuone tu kwani hapa nilipo siwezi kula wala kufanya chochote,"amesema Swahiba
0 Comments