Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako. Picha ya Maktaba
Kwa ufupi
Waliosimamishwa ni Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu (TIA) ambayo ndiyo imepewa idhini ya kusimamia ubora wa vitabu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi vigogo wawili hadi uchunguzi wa sakata la vitabu vya kufundishia utakapokamilika.
Waliosimamishwa ni Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu (TIA) ambayo ndiyo imepewa idhini ya kusimamia ubora wa vitabu
Tanzania imekuwa na tabia ya kutumbua, ila kwenye elimu nadhani hii sio muarobaini kabisa. Elimu ni jambo muhimu kupita kiasi, sio lakukurupukia, Taasisi ya Elimu ni moja ya taasisi kongwe na inayoheshimiwa sana, ila kwa hili inasababisha niseme ni muda muhimu kwa Wizara ya Elimu kukagua wachapishaji wa vitabu nchi nzima.

Wizara ielekee kwenye vyuo vikuu ambapo hujichapishia vitabu vya kiada na ziada, ni hakika kutagundulika mengi.
Upande wa watumiaji lazima wamehathiriwa na vitabu hivi visivyo na ubora, nadhani ni busara wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wa elimu kuombwa radhi kwa kusababishiwa kuletewa kisichobora.
Aibu hii ni haitasafishwa kwa kutumbua bali kukubali, kuomba radhi na kufuatilia kwa karibu zaidi uzalishaji wa Vitabu bora vya ziada na kiada.
Elimu Afrika
0 Comments