Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi. Akizungumzia kuhusu kampeni ya "Weka Akiba na Ushinde na MCB
MWALIMU Commercial Bank PLC imezindua kampeni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.
Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.
“Mteja anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.
Alisema, kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4) na kujishindia zawadi mbalimbali.
Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua kuwa Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi nzima.
“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.
Tunayo Furaha kukufahamisha kuwa Benki ya Mwalimu inaendesha kampeni ya kuweka fedha na kujishindia zawadi,
JINSI YA KUJISHINDIA ZAWADI
1. Kwa mteja aliye na akaunti tayari – weka fedha kiasi cha shilingi 50,000/- na kuendelea
2. Kwa mteja mpya- Fungua akaunti na uweke fedha kiasi cha shilingi 50,000/- na kuendelea.
3. Kwa kila shilingi 50,000/- utakayoweka kwenye akaunti yako inakupa nafasi ya kuingia kwenye droo ya mwezi,
4. Kila mwezi kutakuwa droo na washindi 4 (wanne) watakaojishindia Shopping Voucher na Ipad.
5. Shindano hili ni kwa ajili ya wateja waliopo na wale wapya.
6. Shindano linaanza tarehe 18 Mei mpaka 18 July 2017.
UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUHAMISHA PESA KUTOKA KWENYE SIMU YAKO KWENDA KWENYE AKAUNTI YAKO YA MCB.
1. KWA WATEJA WENYE M-PESA TUMIA UTARATIBU UFUATAO;
a. Piga namba *150*00# kisha chagua namba 6 (Huduma za kifedha)
b. Halafu chagua namba 2 (Mpesa kwenda Benki)
c. Halafu chagua namba 9 (Zaidi).
d. Chagua tena namba 9 (Zaidi)
e. Chagua tena namba 9 (Zaidi)
f. Chagua tena namba 9 (Zaidi) kisha
g. Chagua namba 5 (Mwalimu Bank)
h. Chagua namba 1 (Weka namba ya akaunti), kisha ingiza akaunti namba yako ya MCB, e.g. xxxxxx3101
i. Weka kiasi unachotaka kuhamisha kutoka kwenye simu kwenda akaunti yako ya MCB
j. Weka namba ya SIRI.
k. Bonyeza namba 1 kuthibitisha.
2. KWA WATEJA WENYE TIGOPESA TUMIA UTARATIBU UFUATAO.
a. Piga namba *150*01# kisha chagua namba 6 (Huduma za kifedha)
b. Halafu chagua namba 1 (Tigopesa kwenda Benki)
c. Halafu chagua namba 11 (Other Banks 3).
d. Kisha chagua namba 5 (Mwalimu Bank)
e. Chagua namba 1 (Kuingiza namba ya kumbukumbu), kisha ingiza akaunti namba yako ya MCB, e.g. xxxxxx3101
f. Weka kiasi unachotaka kuhamisha kutoka kwenye simu kwenda akaunti yako ya MCB
g. Weka namba ya SIRI.
h. Bonyeza namba 1 kuthibitisha.
3. KWA WATEJA WENYE AIRTEL MONEY FUATA UTARATIBU HAPO CHINI
a. Piga namba *150*60# kisha chagua namba 3 (Tuma Pesa)
b. Halafu chagua namba 35 (Mwalimu Bank)
c. Chagua namba 1 (Kuingiza namba ya kumbukumbu), kisha ingiza akaunti namba yako ya MCB, e.g. xxxxxx3101
d. Weka kiasi unachotaka kuhamisha kutoka kwenye simu kwenda akaunti yako ya MCB
e. Weka namba ya SIRI.

0 Comments