Bw. Godfrey Mwambe Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika ofisi za kituo hichi jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………….
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Shirika la biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD, limeandaa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo mafunzo ambayo yatafanyika kwa kipindi cha siku sita kuanzia tarehe 26 Juni Mpaka tarehe 01 Julai katika Hoteli ya New Afrika hapa hapa jijini Dar-es-salaam.
Lengo la program hii muhimu na endelevu kwa Wajasiriamali wa Kati (SMEs) na makampuni makubwa ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara hao wadogo ili waweze kufanyabiashara na kutoa huduma kiufanisi na tija zaidi baina yao na hayo makampuni makubwa ya kigeni yaliyopo hapa nchini. Semina hii itawasaidia pia katika kuongeza mbinu na ujuzi katika kuibua fursa mpya, kudumisha biashara baina ya makampuni madogo na makubwa, kuwafundisha namna ya kupata taarifa sahihi za kibiashara, kuongeza ubora na viwango vya bidhaa na huduma wanazotoa na kuongeza ujasiri katika kuendesha biashara zao.
Vilevile lengo lingine muhimu la programu hii ni kuwaunganisha wafanyabiashara hao na wadau mbalimbali yaani BDSPs kama vile taasisi za fedha, wataalam mbalimbali wa huduma za biashara, masoko, biashara na tafiti mbalimbali ili kuwapa ujuzi wa kisekta mbalimbali zinazolenga katika kuboresha bidhaa na huduma zao.
TIC inategemea kuwa baada ya mafunzo hayo wafanyabiashara hao watakuwa wamejengewa uwezo na mitizamo chanya ili baadae waweze kutoa bidhaa na hudumu zinazokidhi ubora na viwango.
Kama Serikali tumekuwa tukihimiza na kutunga sheria na miongozo mbalimbali kuwafanya wawekezaji wakubwa wa nje na wa ndani kutoa fursa kwa makampuni madogo madogo kufanya biashara nao. Lakini mtakubaliana nami kwamba changamoto kubwa ya utekelezaji wa jambo hili ni kushidwa kuwa na uwezo kwa wajasiliamali wetu kufanya biashara na makampuni haya kiufanisi. Mafunzo haya yanalenga katika kusadia kuondoa changamoto hizo.
Mwisho kabisa, napenda kutoa rai kwa wafanyabiashara watakaopata fursa ya kuweza kujengewa uwezo waweze kuzingatia sana mada zitakazotolewa na wawezeshaji hawa. Nina hakika kwa kufanya hivyo tutaweza kuondokana na changamoto za kutokuwa wadau endelevu katika mfumo wa uchumi wetu.
IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI TIC,
0 Comments