WANAFUNZI WA TANZANIA WANG'ARA KITAALUMA MAREKANI

WATANZANIA WANG'ARA MAREKANI.
Wanafunzi watatu wa shule ya sekondari ya FEZA BOYS Dar es Salaam wamenyakua medali za dhahabu huko Marekani katika mashindano ya uwezo wa kitaaluma ya GENIUS OLYMPIAD yaliyoshirikisha nchi 63 Duniani. Walionyakua medali hizo ni wanafunzi Abdulrazak Juma Mkamia,Rashid Jakaya Kikwete na Abdallah Rubeya


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya kimataifa Feza wakiwa na furaha mara ya kuwasilini kutoka nchini Marekani baada ta kushinda medali za dhahabu kwenye mashindano ya Genius Olympiad. Kushoto ni Rashid Jakaya Kikwete, Abdalah Rubeya wakilakiwa na Mhe. Mama Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jana usiku.

Wanafunzi wa shule ya kimataifa Feza wakiwa na furaha mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Marekani waliposhiriki mashindano ya Genius Olympiad.
Mzazi wa Rashid Jakaya Kikwete, Mhe. Mama Salma Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpokea mwanae.
Wanafunzi wa shule ya Kimataifa Feza wakiwa pamoja na wanafunzi na wazazi wao mara baada ya kuwasili mara ya kuwasili kutoka nchini Marekani baada ya kushinda medali za dhahabu kwenye mashindano ya Genius Olympiad katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jana usiku.

0 Comments