Mh Rais, ili Tanzania ya Viwanda itekelezeke kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo basi #Somolakilimo lirejeshwe mashule hasa #Msingi na #Sekondari.
Hatuwezi kuwa na viwanda bila kuwa tunazalisha malighafi ya viwanda vyetu wenyewe, ili viwanda viwe vya kudumu, watanzania wazalishe malighafi kwa wingi wa kutosha viwanda vyetu ili kupunguza bei ya bidhaa zitakazozalishwa.
Mimi nilisoma #Kilimo na nakiri Elimu niliyoipata inanisaidia sana katika maisha ya kawaida, nimetembelea Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) nimeona umuhimu wa kuanzia uwekezaji wa taaluma yetu hii kuanzia shule ya msingi na sekondari ili kuwa uelekeo bora kwenye vyuo na vyuo vikuu.
Nakumbuka kuwa #Kilimo ni #Uti wa mgogo wa uchumi wa nchi. Nakumbuka kauli mbiu ya #Kilimo ni #Siasa.
Kwa kukataza #Kilimo kufundishwa shule za msingi na sekondari ni sawa na kuvunja kiuno cha mwanadamu na kutegemea mgongo, shingo n kichwa kufanya kazi vema.
Uti wa mgongo wa uchumi wa watanzania zaidi ya 85% ni #Kilimo ila kwa kukosa Elimu ya msingi ya #Kilimo cha kisasa tija imekuwa ndogo sana.
Nashauri Wizara ya Elimu itafakari ushauri huu na kuchukua hatua ili Tanzania iwe na Uchumi wakujitegemea kimalighafi.
Tufuatilie kupitia, Instagram: @elimuafrika, Facebook: Elimu Afrika, Twitter: @ElimuAfrika na YouTube: Elimu Afrika
#SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments