SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Leo ni kumbukumbu ya vifo vya kinyama kuwahi kutokea katika historia ya Afrika na Dunia kwa ujumla.

Siku kama ya leo watoto wa shule za watu weusi Afrika Kusini waliamua kuchukua hatua ya kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa umeidhinishwa na Sera mbaya ya "Apartheid".

Sera hiyo ya ubaguzi iliwanyanyasa na kupuuza UTU wa mwafrika, hivyo waafrika wakaamua kudai kwa njia mbalimbali ikiwemo hii ya watoto wa shule.

Tunajifunza kuwa lazima tujenge ujasiri, uelewa na shauku ya kudai haki, usawa na heshima kwa watoto wetu, ukandamizaji, ubaguzi na unyanyasaji  wowote tutakaouvumilia watoto wetu wasiuvumilie.

Kweli waliuwawa na polisi wa kikaburu wa Afrika Kusini ila leo dunia inaadhimisha ushujaa walioufanya, #Tujengeujasirikwawatoto.

Elimu Afrika inaungana na watanzania, waafrika na dunia kwa ujumla kuadhimisha  siku hii ya #WatotoMashujaa wa Afrika

Elimu Afrika

0 Comments