TAASISI ZA VIJANA ZATOA ELIMU YA UZAZI KWA VIJANA WENZAO


Wanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) na Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania Penina Mgonela (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Mwanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyikiti wa Taasisi ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) chairperson William Otuck baada ya kutia saini ya makubaliano ya kufanya kazi chini ya taasisi hiyo yenye lengo ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Jumla ya taasisi kumi za vijana zimeungana ili kuzidisha nguvu ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania na zaidi ikilenga matumizi ya mpango wa uzazi. Vijana hao wamejizatiti kuhahakisha kuwa kuna uwekezaji wa kutosha kwenye elimu juu ya uzazi wa mpango na pia vijana kuhusisha kwenye maamuzi yanayohusu vijana na afya ya uzazi.

Taasisi hizo zimetiliana saini makubaliano na kuwa taasisi moja ikayoitwa Tanzania Adolescent and Youth Reproductive Health (TAYAHR) jana jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye kutoa elimu, kuhusisha vijana na kuhakikisha huduma inafika kwenye maeneo sahihi kwa muda sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TAYAHR William Otuck alisema Tanzania ina changamoto kuona ya kwamba asilimia 27 ya vijana wenye miaka 15-19 wana mtoto au ni wajawazito huku utumiaji wa uzazi wa mpango na hasa vidonge vya uzazi kati yao ikiwa ni chini sana – yaani asilimia 13 peke yake huku pia wakiwa hawana elimu yeyote kuhusu afya ya uzazi na hivyo kukosa uamuzi sahihi kwenye masuala ya kujamiiana.

‘Robo ya wasichana wenye umri kati ya 15 na 19 Tanzania wana watoto au ni wajawazito na hali ni mbaya kwenye mkoa wa Katavi yenye asilimia 45 na Tabora asilimia 42 kwa wasichana wenye umri huo. Hii inamaanisha kuna idadi kubwa ya wasichana ambao wanakatisha masomo na kuingia kwenye hali ya kuwa mzazi wangali wana umri mdogo na hii kwa kiasi kikubwa uchangia kuongeza hali ya umasiki kwenye jamii’, alisema Otuck huku akiongeza kuwa idadi kubwa ya wasichana wadogo wakipata mimba pia kunachangia kuongezeka vifo vitokanavyo na uzazi.

Akizungumzia kuhusu elimu na hali ya kupata mimba za utotoni, Otuck alisema tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia 10 wa wasichana ambao wana elimu mpaka ya sekondari ambao hupata mimba wakiwa na umri mdogo kulinganisha na wale wana elimu ya msingi ambao ni asilimia 34 na wale ambao hawana elimu kabisa ni asilimia 52.

Taasisi hiyo chini ya uongozi wa vijana pia imelenga kuhamasisha wenye kutoa maamuzi (policy makers) kuwekeza kwenye kupanua wingo la matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango ili kufikia walengwa ambao bado hawajafikia, ambapo kwa sasa inaonyesha asilimia 23 ya wanawake vijana wanatamani kutumia uzazi wa mpango lakini bado huduma hiyo

haiwajafikia na pia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango kwa vijana angalau kufikia asilimia 80 ifikapo 2010 na pia kuendeleza elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.

Taasisi hizi kabla ya kufikia makubaliano yao zilianza mazungumzo mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana chini ya FP2020 Secretariat, mradi wa Advance Family Planning (AFP) Tanzania pamoja na taasisi ya Torchlight Collectives. TAYAHR inaundwa na taasisi za Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania, YAM-UMATI, AfriYAN, TYVA, SAYI, Restless Development, Zanzibar Youth Forum (ZAFAYCO), IYAFP/Young and Alive Initiative (YAAI), SHDEPHA+ na YUNA.

0 Comments