Tulipata fursa ya kutembelea Chuo Kikuu cha SUA kitengo cha Mafunzo ya Panya Buku (APOPO).
Kitengo hiki kinafundisha Panya Buku kugundua Mabomu yaliyochimbiwa ardhini, nimeelezwa na kushuhudia Panya hawa wanavyofundishwa hatua kwa hatua mpaka wanakuwa wabobezi wa ugunduzi wa mabomu ya ardhini.
Mara ya kwanza nilikuwa nasikia eti Panya wanagundua mabomu sikuelewa, kwa sasa nimeelewa, nimejifunza na niwaambie watanzania, waafrika kwa ujumla tuchague kutembelea maeneo tofauti na sehemu za starehe, kama Apopo kwakuwa wawezatembelea eneo kama hili ukaburudika, elimika na kupata cha kurithisha kizazi cha sasa na kijacho. Ni ajabu na aibu wenzetu wanatoka nchi zingine kuja kujifunza, sisi atuthamini, nadhani tujitahidi kuhamasika kuthamini vyetu.
Tuwapongeze vyombo vyetu vinavyohusika kuwawezesha Apopo kufanikisha mafunzo na vitendea kazi vya kazi hii kubwa ya kujali maisha ya wanaadamu duniani. Tunawashukuru uongozi mzima na watumishi wa Apopo SUA-Morogoro kutupokea kwa Hekima na kutupa Elimu ambayo tuitegemea na zaidi ya matarajio yetu.
Ni fursa kwa wanafunzi, vijana na watu wazima kutembelea APOPO ili kujifunza na kujionea vipaji vya walimu wenye maarifa ya kuwafundisha Panya Buku ambao wanaiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali ya dunia kwenye kazi maalumu ya kiusalama ambayo nia ni kuwezesha dunia kuwa salama.
"Jitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wako na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote"
Shukrani
Elimu Afrika inapenda kuwashukuru APOPO kwa kujitolea kuelimisha, kuokoa maisha, mmethibitisha Uzalendo, Utayari wenu kuitumikia dunia, hivyo mmefuzu Thamani ya kuwa Tunu/Urithi wa Dunia.
Asante sana
Mr Daniel
Founder/CEO
Tufuatilie kupitia, Instagram, Facebook, Twitter, YouTube
#SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments