JE WAJUA?

Je wajua?
Kwa picha hii;
Nchini Japani watoto huanza kufanya mitihani darasa la NNE. Kwasababu nia ya elimu ya awali si kupima uelewa na maarifa ya mtoto, bali kujenga tabia njema na kukuza maadili. Hivyo wao kwa miaka mitatu hutumia kuwajengea #Maadili bora na adabu.

Kama nchi lazima tuanze kutafakari kuhusu uelekeo wa Elimu yetu, wakati tukijenga uelewa na maarifa, tukumbuke umuhimu wa #Maadili kupitia kujenga tabia njema na malezi yanayojenga Utu, Upendo na Uzalendo.

"Jitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wako na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote"

Tufuatilie Elimu Afrika kupitia, Instagram, Facebook, Twitter na YouTube.

#SiasaIsiingilieTaaluma.

0 Comments