TAFAKURI YA MWALIMU


Kila Shule ya Msingi na Sekondari inapoanzishwa huwa inakuwa na "Falsafa" yake, mara nyingi waanzilishi wa shule ndio huwa chanzo cha falsafa hizi za shule, wanafunzi wanapoanza kusoma kwenye shule hizi huishia kuzisoma kwenye vibao vya shule na machapisho yenye nembo na falsafa hizo.

Nishauri kwenye uandikishaji na kila mwanzo wa mwaka ni vema shule zote zikatenga siku moja ya kueleza kwa kina falsafa ya shule husika na kuirejea kwa mwaka mara moja ili kujenga imani ya kuishi falsafa ya shule kwa vitendo hasa baada ya kuhitimu ngazi husika toka shule husika.

Wanafunzi wasisitizwe kuelewa Falsafa ya shule na kuelezwa namna ya kuiweka kwenye vitendo ndani ya shule, nje ya shule na baada ya kuhitimu.
Elimu Afrika

0 Comments