Darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa.
Wazazi wakishudia makabidhiano ya darasa lenye thamani ya Milion 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa.
Kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania Tigo, leo imekabidhi darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi iliyoko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma katika juhudi za kusaidia ukuaji wa kiwango cha elimu wilayani humo.
Akiongea katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema kwamba mchango huo ulikuwa ni sehemu ya juhudi za wafanyakazi wa Kampuni kujitolea na jukumu la kampuni kusaidia maendeleo ya jamii (CSR) katika kusaidia elimu Tanzania.
“Tigo ina sera nzuri ya (CSR) ambayo inasisitiza katika kutoa kwa ajili ya kusaidia Jamii ambako kampuni inaendesha shughuli zake. Tunaamini kwamba kupitia mchango huu, Tigo itakuwa imechangia kwa mara nyingine katika kutengeneza mazingira kwa ajili ya ukuaji wa wataalamu wa baadae kwa ajili ya maendeleo ya haraka ya nchi”, alisema Lugata.
Katika nafasi yake Meneja wa CSR wa Tigo, Bi Halima Okash, aligusia vipaumbele vya kampuni vya uwekezaji katika jamii, akisema kwamba Tigo ilikuwa tayari kushirikiana na wadau wengine wenye fikra kama hizo katika juhudi zake za kusaidia maendeleo ya jamii.
Kupitia mpango wetu wa uwekezaji katika jamii, Tigo imekuwa katika mstari wa mbele kuinua sekta ya elimu nchini ambapo tumeshatoa komputa na kuunganisha shule 60 za sekondari kwenye mtandao wa intaneti wenye kasi zaidi kupitia mradi wetu wa e-school pamoja na kuchangia zaidi ya madawati 7,000 kwa shule za msingi nchini kote”alisema Okash.
Mgeni rasmi katika sherehe, Mkuu wa mkoa wa wilaya ya Kondoa, Sezeria Makutta aliishukuru Tigo kwa mchango wake, akibainisha kwamba itasaidia sana katika kupunguza msongamano wa wanafunzi katika darasa moja, ambapo itatengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia shuleni.
“Tunawashukuru sana Tigo kwa msaada wao”, alisema Makutta, akiongeza kwamba; “Tunawaomba watu wengine wenye moyo wa kujitolea kujitokeza na kuongeza nguvu katika kuondoa upungufu wa madarasa katika wilaya yetu”.
0 Comments