TUTAFAKARI ELIMU YETU

Kwa miaka mingi kumekuwa na maboresho na majaribio ya namna mbalimbali kwenye sekta ya Elimu kwa kuwa ni wazi mfumo wetu unashindwa kushindana vema ki ubora na ki ualisia na mifumo ya nchi zingine za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kwa ushaidi ni matokeo ya kidato cha NNE kwa mwaka jana yalionyesha mfululizo wa mkwamo wa ufaulu hususani shule za umma ambazo idadi kubwa ya wanafunzi huwa ni watoto wa maskini
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 NECTA matokeo yalionyesha ufaulu na ubora wa Elimu kushuka kwa 1. 85% kutoka 69.75% ya mwaka 2014 hadi 67.91% ya mwaka 2015.

Kwa maoni yetu;
Ili ufaulu na ubora wa elimu kwenye shule za umma uboreke basi sharti jamii, wadau, wanafunzi na serikali ijipange kwa vitendo kupunguza au kukabiliana na changamoto zifuatazo;

Upangaji wa wanafunzi uzingatie ufaulu wa juu kwenda shule za umma sio wale wenye ufaulu wa juu kwenda shule binafsi.

Mazingira ya kazi ya walimu yaboreshwe ili kusababisha hamasa ya kazi ili kuleta matokeo mazuri, shule za umma maeneo mengine walimu wanakalia ndoo au matofali.

Idadi kubwa ya wanafunzi kwenye madarasani baadhi ya shule za umma ni wanafunzi 65-100 kwa mkondo.

Wanafunzi wa shule binafsi wanatumia mabasi kwenda shule na kurudi nyumbani, wanakunywa chai na vitafunio, wanapata chakula mchana wanafundishwa walimu wakiwa wamepunguziwa msongo wa mawazo, lazima wafaulu bila maelezo.

Shule za umma usafiri kwa walimu kuja kazini na kurudi nyumbani ni ngumu, chai na vyitafunio na chakula cha mchana ni hanasa. Ki ukweli baadhi ya walimu wanakosa hata nauli ya kuja shule na kurudi kwa mwezi mzima, kodi za nyumba ni mzigo kwao alafu hawa walimu utegemee nini toka kwao.

Vifaa vya ufundishaji na kujifunzia mfano vitabu, maktaba, maabara na vyumba vya kompyuta vyote ni ni kitendawili, kwingine wanasomea chini miti.

Taaluma inaingiliwa walimu wamekosa furaha, wamekata tamaa, wanafedheheshwa , wanadhalilishwa, wanadharauliwa, wanapuuza na kushushwa thamani na baadhi ya viongozi ilhali walimu haohao wanategemewa walete ufaulu ni ndoto.

Tafakari ifanyike kwenye Lugha ya kufundishia kuanzia darasa la Awali hadi la saba. Wanafunzi wawe kutoka pande mbalimbali kusomea shule moja ili uelewa uwe wa tofauti (mfano isiwe lazima mwanafunzi anaesoma Ngarenaro msingi apangiwe Ngarenaro Sekondari).

Serikali ya Tanzania iige Serikali ya Ujerumani kuhusu maslahi na mishahara ya walimu ambayo Walimu ndio wanaolipwa mishahara na maslahi bora kuliko kada zingine zote. Kwa kuanzia walimu walipwe mshahara wa Mbunge ili manung'uniko ya walimu yasiwagaribu wanafunzi.

Ninadhani ni wakati muafaka kufikiri kwa kina uelekeo wetu kama nchi katika suala la ubora wa elimu.

Elimu Afrika

Tufuatilie kupitia Elimu Afrika Instagram, Facebook, Twitter,YouTube na
www.elimuafrikatz.blogspot.com #SiasaIsiingilieTaaluma.

0 Comments