VYUO VIKUU VYA KENYA VYAFUNGWA KWA KUKOSA WANAFUNZI

Waziri wa Elimu wa Kenya ameamuru kufungwa kwa matawi ya vyuo vyikuu nchini Tanzania na Rwanda. Vyuo hivyo ni Kenyetta University na Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology.

Waziri huyo amelazimika kufikia uamuzi huo baada ya kukumbwa na ukata wa wanafunzi kutokana na maelekezo ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuwanyima fursa za ushindani wa kupata wanafunzi.

Tume hiyo ilitoa uhuru kwa wanafunzi kuchagua vyuo wenyewe badala ya mpango wa awali wa kuwadahili na kuwapangia vyuo mbalimbali kutokana na utashi wa tume, kinyume na sasa ambapo wanafunzi huchagua wenyewe na mazingira kuonyesha wengi huchagua vyuo vya serikali au vya taasisi za dini za hapa nchini.

Hivyo uhaba huo wa wanafunzi unaokabili vyuo hivyo ndio sababu kubwa ya kufunga matawi haya nchini Tanzania.

0 Comments