WANAFUNZI WALEMAVU WAKUMBUKWA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya amemuagiza msimamizi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Kantalamba kuhakikisha kuwa walemavu wanajengewa vyoo vyao ndani ya mabweni wanamolalia nia ikiwa ni kujiepusha na kuwaamsha wenzao usiku pindi wanapotaka kwenda chooni.

Mhandisi Manyanya ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule hiyo iliyopo Wilayani Sumbawanga iliyopewa shilingi Bilioni 1.1 ikiwa ni mpango wa serikali wa kuzirudishia hadhi shule kongwe nchini huku shule hiyo ikiwa ni ya tangu 1964.

“Lazima muhakikishe kwamba mnakuwa na vyumba maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu na kuwawekea miundombinu hasa kwa wale walemavu ambao mazingira yao ni magumu zaidi, kwa mfano mwanafunzi ana ulemavu wa miguu na anatakiwa kwenda chooni hapaswi kutambaa kwenye mikojo ya wanafunzi wenziwe hii inawapelekea wao kuwa katika mazingira hatarishi zaidi,” amesema Manyanya.

Mbali na agizo hilo  Mhandisi Manyanya ametoa wiki tatu ukarabati wa shule hiyo kumalizika baaada ya muda waliopangiwa kumalizika huku kipaumebele kikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao katika hali ya utulivu.

“Sijaridhishwa na kasi ya ukarabati huu hivyo tumewaongezea wiki tatu mhakikishe mnamaliza ili wanafunzi waendelee na masomo maana yake kama mngekuwa hamwezi kumaliza kwa wakati kwanini msingesema mapema", amesisitiza Manyanya.

Kwa upande mwingine, Mhandisi Manyanya amewasisitizia wanafunzi wa shule hiyo kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa hakuna tofauti kati ya shule za serikali na za binafsi kuanzia huduma za majengo, elimu mpaka vifaa vya kusomea

0 Comments