Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage
Kwa ufupi
Akizungumza leo (Jumanne, Julai 4), Mwijage amesema kiwanda hicho kikitengeneza viatu vya bei nafuu kitapata masoko na hivyo kutoa ajira kwa wananchi.
Dar es Salaam. Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage amekitaka kiwanda cha kutengeneza viatu cha Bora kutengeneza viatu vya bei nafuu kwa ajili wanafunzi ili wasitembee peku.
Akizungumza leo (Jumanne, Julai 4), Mwijage amesema kiwanda hicho kikitengeneza viatu vya bei nafuu kitapata masoko na hivyo kutoa ajira kwa wananchi.
Ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuzalisha viatu vyenye ubora ili vishindane na vinavyotoka nje ya nchi.
"Mkitengeneza viatu vyenye ubora na vya bei nafuu watu wataacha kuvaa viatu vya mtumba vyenye fangasi," amesema.
0 Comments