Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Anna Gidarya amefanya ziara kwenye Wilaya za Mkoa wa Manyara katika ziara hiyo ametembelea Shule ya msingi Endanoga iliyopo Kata ya Galapo, ili kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya Elimu Mkoani kwake.
Katika kuchangia kwa vitendo utatuzi wa changamoto zinazowakabili wanafunzi na walimu shuleni hapo Mh Mbunge amechangia Fedha taslimu shilingi 1,250,000/= kwaajili ya kuweka vioo kwenye madirisha ya shule na ununuzi wa viti bora vya walimu.
0 Comments