ZIKO WAPI NYIMBO ZA UZALENDO?


Shule zote nchini huimba wimbo wa Taifa, imefikia mahali wameuzoea na kuuimba ili kutimiza wajibu tu lakini ukiwatazama waimbaji huoni tafakuri ya maneno toka kwenye vilindi vya roho.

Hawaonyeshi kuipenda Afrika acha Tanzania yetu, nakumbuka nyimbo mbalimbali tulikuwa tukiziimba tukiwa shule ya msingi kwenye mchakamchaka na mstarini mfano; Tanzania, Tanzania, Tazama ramani, Mchakamchaka chinja, IDD Amini n.k

Pamoja na ugumu wa maisha ila tusipuuze Uzalendo wa nchi yetu, turejeshe nyimbo hizi zakizalendo kwenye shule zetu kwa kasi.

Tumefikia nyakati ambazo shule zinasisitiza wanafunzi kuimba wimbo wa shule zaidi ya wimbo wa Taifa na kusahau kabisa nyimbo za kizalendo, nikumbushe walimu wote kuwahadithia enzi za Mwalimu Nyerere na Mwinyi msisitizo wa uzalendo ulivyokuwa mashuleni na idara zote.

Hatujachelewa turejee kwenye uzalendo tuliourithi toka kwa waliotutangulia ili kizazi kijacho kirithi kilichobora pia.
Elimu Afrika

0 Comments