WHEELS - AFRICA YATOA MAFUNZO YA UDEREVA WA BIASHARA KWA WANAWAKE


Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya udereva wa kibiashara ambao utawawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

Bw. Martin Gabone amesema Semina hii ina lengo la kuwaandaa wanawake watanzania na Afrika kwa ujumla kupata ujuzi katika taaluma ya udereva wa kibiashara ambapo wanawake hawa watapata mafunzo maalum katika programu ya Women On Wheel - Africa ili kujiwezesha na kujitegemea kiuchumi kupitia taaluma hii ya udereva wa kibiashara na wenye tija kwa maisha yao na taifa kwa ujumla wake.

Women On Wheel - Africa inawakaribisha wanawake akina mama kwa wasichana kujisajiri ili kujiunga na mpango huu muhimu ambapo mafunzo yanatarajiwa kuanza mwezi wa tisa mwaka huu 2017 jijini Dar es salaam katika ofisi za taasisi ya

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba hizi.

0712 156 933: 022 2664618: 022 2664587

OFISI ZA TAASISI HIYO ZIPO KINONDONI ADA ESTATE KARIBU NA BAKWATA HIGH SCHOOL

 

Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ofisi za Women On Wheel - Africa Kinondoni.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ofisi za Women On Wheel - Africa Kinondoni.

Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

 

Mjasiriamali Bi Tedy Daniel mmoja wa washiriki wa semina hiyo akifafanua jambo kwa wanasemina wenzake wakati wa mafunzo hayo.

Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akiwaelekeza jambo baadhi ya washiriki wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji

0 Comments