ELIMU YA UFUGAJI NYUKI

Mkufunzi wa mafunzo ya ufugaji nyuki Baltazar Lylimo akitoa maelezo kikundi kilichopo kijiji cha Ketumbeini,Wilaya Longido Mkoani Arusha kuhusu namna mizinga inavyoweza kuhifadhi Asali nyingi endapo watafuata maelekezo ya ufugaji,Kulia ni Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi ya kaskazinikati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri(Picha na Pamela Mollel Arusha)

Wanakikundi wakishuhudia mzinga wa nyuki ukiwa juu ya mti mara baada ya kufundishwa njia bora ya ufugaji nyuki katika kijiji cha Ketumbaine

Wilayani Longido Mkoani Arusha.

Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania (KKKT)Dayosisi ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri akizungumza na viongozi wa kikundi cha ufugaji nyuki.

Mratibu wa miradi ya kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi

ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Simon Sandilen akizungumza na vyombo vya habari juu ya semina ya ufugaji nyuki.

Wanakikundi wakishuhudia mzinga wa nyuki ukiwa juu ya mti mara baada ya kufundishwa njia bora ya ufugaji nyuki katika kijiji cha Ketumbaine Wilayani Longido Mkoani Arusha.

Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri akizungumza faida za ufugaji nyuki.

Mkufunzi wa semina juu ya ufugaji nyuki, Baltazar Lyimo kusoto akiwaonyesha wanakikundi vazi maalumu la kuvaa wakati wa uvunaji asali.

Muonekano wa eneo hilo katika picha.

 

Jengo la kanisa.

Picha ya pamoja baada ya semina ya ufugaji nyuki.

Zaidi ya wanakikiundi 150 katika kijiji cha Ketumbaine Wilayani Longido Mkoani Arusha, wamepatia semina ya ufugaji nyuki itakayowasaidia kujipatia kipato sambamba na chakula.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Mratibu wa miradi ya kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)Dayosisi ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Simon Sandilen alisema kuwa mradi huo unathamani ya shilingi Milioni tatu.

Alisema kuwa Asali mbali na kutumiwa kama chakula pia hutumika kama dawa hivyo ni vyema wanakikundi wakafundishwa njia za kisasa za ufugaji nyuki ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umasikini.

Hata hivyo alisema kuwa jamii hiyo ya kimaasai itaweza kunufaika na semina hiyo ya siku moja kwa kujua mbinu zitakazowawezesha kuwaongezea kipato kwa muda mfupi ukilinganisha na miradi mingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania (KKKT) Dayosisi ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri alisema kuwa mradi huo umefadhiliwa na kanisa la kilutheri la huko Ujerumani.

Alisema kuwa mradi huu utasimamiwa kikamilifu pamoja na miradi mingine itaendelea vizuri na italeta matokeo mazuri yaliyokusudiwa kwa kuwa uongozi unaosimamia hiyo miradi upo imara.

Mnufaika wa semina hiyo ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Joseph Ndila alishukuru kwa semina hiyo huku akisema elimu waliyoipata wataweza kuwaelimisha na wafugaji wengine.

“Aliongeza kuwa ufugaji wa awali haukuwa wa kisasa kwakuwa walikuwa wakiua nyuki bila sababu lakini leo tumefundishwa njia sahihi za kurina asali na vifaa muhimu vya kutumia katika uvunaji asali”alisema Ndila

Naye Mkufunzi wa semina hiyo Baltazar Lyimo alisema kuwa wananchi wa eneo hilo wanarasilimali miti ambayo itawawezesha wafugaji hao kuweza kupata asali nzuri

“Elimu ya ufugaji nyuki kwa huku umasaini bado elimu hii haijasaamba ukilinganisha na maeneo menginealisema Lyimo.

0 Comments