SIMANZI TENA ARUSHA


 

Wakazi wa jiji la Arusha waliokusanyika kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika kushuhudia uopoaji wa miili ya watoto wawili kwenye shimo.Picha na Filbert Rweyemamu

By Filbert Rweyemamu, Arusha

Kwa ufupi

Shimo hilo lipo kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika.

Arusha. Miili ya watoto wawili ambayo haijatambuliwa imeopolewa shimoni eneo la Mji Mpya katika Mtaa wa Olkerian jijini Arusha.

Mwenyekiti wa mtaa huo, uliopo Kata ya Olasiti, Daudi Safari amethibitisha tukio hilo lililovuta wananchi wengi waliojitokeza kushuhudia kuopolewa kwa miili hiyo.

Kazi ya uopoaji ikitekelezwa na  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Shimo hilo lipo kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika.

0 Comments