Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” jijini Dar es Salaam
Kwa ufupi
Waklimu wanaofundishwa watatumika kuwafundisha wanafunzi
Mafunzo yatawawezesha wajasiriamali kutumia teknolojia vizuri kwenye shughuli zao.
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya teknolojia na habari na mawasiliano (Tehama) kwa waalimu mkoani Dar es Salaam
Mafunzo hayo yanafanyika katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama katika Manispaa ya Kinondoni.
Walimu wanaopatiwa mafunzo hayo ni walimu vijana wa ngazi za shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu.
Pamoja na walimu mafunzo hayo pia yanatolewa kwa wafanyabiashara.
Taarifa iliyotolewa na Airtel inaeleza kuwa mafunzo yatawasaidia kuvumbua aplikesheni mbalimbali kwenye simu, kuwapatia ujuzi katika maswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia teknologia za kisasa
“Awali tulikuwa tulitoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni bora na waalimu wa nao wanufaike. Hii itasaidia sana kwa sababu baadaye wao ndio watakuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi. Hilo likifanyika, litayuipa nafasi kuednelea na shule nyingine,” amesema Meneja Mradi wa Airtel, Jane Matinde.
Waalimu walio katika mafunzo hayo wameonyesha kuyafurahia na wameonyesha hamasa kubwa.
Hata hivyo, Matinde amrsema kuwa mafunzo kwa wanafunzi yataendelea kwa wale ambao tayari walikuwa wameshaanza.
Aliongeza kuwa bado wanapokea maombi ya kujiunga na akatoa wito kwa vijana kutoka shule za sekondari, wale waliomaliza darasa la saba na wafanyabiashara kutumia vyema maabara hiyo yenye lengo la kuwezesha jamii hususani vijana kuongeza ujuzi na weledi kwenye maswala ya teknologia.
Kwa upande wake Meneja wa maabara hiyo, Agape Jengela alisema: “Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama. Tuhahakisha kuwa walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao waanze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi
0 Comments