MAMBO YA KUZINGATIA UKITAKA KUSOMA NJE YA NCHI

Kwa ufupi

Nakubaliana na wanaotamani kusoma nje ya nchi baada ya kumaliza shahada ya kwanza.

Vijana wengi kama wewe wenye ndoto za kufika mbali kielimu wanatamani kusoma nje ya nchi. Nakubaliana na wanaotamani kusoma nje ya nchi baada ya kumaliza shahada ya kwanza.

Faida ya kumaliza shahada ya kwanza hapa nchini ni kuepuka ulazima wa kujifunza lugha ya nchi husika hasa kama nchi hiyo Kiingereza si lugha ya kwanza ya mawasiliano.

Mara nyingi katika nchi ambazo hazitumii lugha ya Kiingereza, hutumia lugha zao kufundishia katika daraja hili, baadhi ya nchi hizo ni Ujerumani, Ufaransa, Sweden, Denmark na China.

Hivyo, mwanafunzi atalazimika kusoma lugha hizo, kufanya mitihani akifaulu ndiyo aendelee na masomo.

Tofauti na wanaokwenda kwa ajili ya kusoma shahada ya pili na ya uzamivu kwa daraja hili zinatumia lugha ya Kiingereza kufundishia.

Ili kuepuka kupoteza muda wa mwaka mmoja au miwili bora kusoma shahada ya kwanza hapa nchini kabla ya kuomba ufadhili.

Kuna mambo kadhaa yanayofaa kuzingatiwa kwa mujibu wa maelezo yatolewayo na vyuo mbalimbali vya nje vinavyotoa ufadhili wa masomo.

Mwanafunzi au mwombaji anapaswa kwanza kutafuta chuo ambacho kulingana na sifa alizonazo atakubaliwa kujiunga nacho.

Kupata chuo kabla ya kutafuta ufadhili ni muhimu ili kumuhakikishia anayekulipia hata kama ni chuo chenyewe kuwa umekidhi vigezo.

Hii itamsaidia mfadhili au chuo husika kufahamu gharama za masomo yako, lakini kwa wanaosomeshwa na wafadhili hili

litawasaidia kukulipia kupitia moja kwa moja katika chuo husika, kwa sababu wapo wafadhili hawatoi fedha wanalipia gharama moja kwa moja.

Kabla hujawa na fikra za kuomba ufadhili, hakikisha unasoma kwa bidii na kupata matokeo mazuri, kwa sababu ndiyo kigezo

cha kwanza cha kupata ufadhili wa masomo.

Usisahau pia kuwa na weledi wa kujieleza hususani kwa kile unachokwenda kufadhiliwa kusoma, kwa sababu wengine unapoomba

ufadhili kuna nyaraka unatakiwa ujaze za kulielezea hilo.

Jambo lingine la msingi ni kuwa na weledi katika kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya Kiingereza.

Kama tulivyosema hapo awali nchi nyingi hutumia lugha hiyo pekee kufundishia, hivyo kama unababaisha babaisha itakupa

taabu kwenda sambamba nao.

Ndiyo maana ninasema kwa shahada ya pili na kuendelea itakuwa bora sana wakaomba hizo nafasi kwa sababu watakuwa na muda wa

kunoa kimombo cha hata baada ya kumaliza shahada ya kwanza.

Kabla ya kuomba ufadhili huu pia hakikisha unaboresha mawasiliano. Jiandae kikamilifu kwa sababu unaweza kutumiwa maswali au nyaraka za kujaza kupitia barua pepe.

Pia unaweza kutakiwa kufanya mawasiliano ya ana kwa ana, kwa njia ya simu , yaani kwa kifupi usiwe mtu wa kubabaika katika

kujieleza.

Unapojaza maombi ya ufadhili lizingatie sana hili. Usikimbilie kumaliza kujaza kila fomu unayopewa. Jaza kila kitu usiche hata kimoja, lakini fanya hivyo kwa usahihi na umakini wa hali ya juu.

Katika hili halihitaji ujanja ujanja wa Bongo, kila kitu unachoulizwa kina manufaa kwako na kwao siku zijazo hivyo jaza kila unapotakiwa kufanya hivyo tena kwa kuelewa ulichoulizwa

na siyo vinginevyo.

Hayo ni machache miongoni mwa mengi unayotakiwa kufanya kabla ya kuomba ufadhili wa masomo nje ya nchi, lakini pia unapochagua chuo linganisha gharama wakati mwingine unaweza kupata ufadhili wa nusu gharama.

Ushauri wa kuzingatia usiombe ufadhili katika chuo kimoja.

Kama kuna changamoto jipange jinsi yakukabiliana nazo, kwani ndio mwanzo wa kuwa na ujasiri katika uthubutu

0 Comments