MH MBUNGE ATOA MSAADA KWA WALEMAVU - SHINYANGA

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal  akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika shule ya msingi.

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) ametembelea shule ya msingi aliyosoma Tinde iliyopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga kisha kutoa msaada kwa wanafunzi nane wenye ulemavu wa viungo akiwemo kijana ambaye hawezi kuongea wala kutembea. 

 

Mbunge huyo ametembelea shule hiyo jana Jumatano Septemba 27,2017. 

 

Mheshimiwa Hilal ametoa msaada wa baiskeli kwa kijana ambaye hawezi kutembea wala kuongea anayesoma katika shule hiyo huku akijitolea kuwanunulia wanafunzi hao nane mahitaji yao yote ya shule mpaka watakapomaliza masomo yao ya shule ya msingi. 

 

“Hii shule nimesoma,baada ya kufika hapa nimeambiwa kuna watoto wenye ulemavu,baada kumuona kijana huyu nimempatia baiskeli lakini pia nimejitolea kuwahudumia wanafunzi hawa wanane ambao wana ulemavu wa viungo,nitawanunulia mahitaji yao ya shule na watakuwa wanakunywa uji kila siku kwa gharama zangu”,ameeleza Mbunge huyo. 

 

Mbali na kutoa msaada huo Mheshimiwa Azza Hilal ameshiriki zoezi la Upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga lililoanzishwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro lenye kauli mbiu ya “Shinyanga Mpya, Mti Kwanza”. 

 

Akiwa katika kata ya Tinde,mbunge huyo aliungana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kupanda miti katika shule ya msingi Tinde,pia katika barabara kuu ya kutoka Tinde kwenda Kahama na barabara ya kutoka Tinde kwenda Nzega mkoani Tabora.

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal  akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi Tinde,aliyeshikilia kipaza sauti ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akiwa na mwanafunzi aliyepata msaada wa baiskeli kutoka kwa Mheshimiwa Azza Hilal

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akipanda mti katika shule ya msingi Tinde.

0 Comments