Taasisi isiyo ya kiserikali “TYCEN” Tanzania Youth Culture Exchange Network inayojishughulisha na maendeleo ya vijana kupitia miradi ya kijamii inayofanyika ndani na nje ya Tanzania hususani miradi ya sanaa, utamaduni, elimu, ujasiriamali, jinsia , Afya, utunzaji mazingira na maendeleo endelevu , imefanikisha kuanzishwa kwa “TYCEN CLUB” katika shule za sekondari zilizopo Nchini.
Klabu hizo kwa mujibu wa waratibu wa TYCEN wameeleza kuwa wameweza kuanzisha katika Manispaa ya Kigamboni, miongoni mwa shule zilizofikiwa kwa sasa ni, shule ya Sekondari Malela, Mikwambe na Changanyikeni.
Imeelezwa kuwa, lengo kubwa la kuanzishwa kwa Club katika shule hizo ni kuwapatia wanafunzi fursa zinazopatikana kupitia TYCEN kutoka mashirika tofauti tofauti yaliyomo ndani na nje ya nchi, vile vile kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini kwa kushiriki katika matamasha na matukio kama vile semina, mashindano ya uandishi wa Insha, mafunzo ya kitamaduni na mambo mbalimbali.
Aidha, mbali na hayo kwa sasa wanafunzi wa shule hizo wanapatiwa mafunzo ya “Life skills” kama vile njia mbadala za kutatua migogoro wanayokumbana nayo katika maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya Wanafunzi waliopo kwenye klabu hizo wakifuatilia mijadara inayoendelea
0 Comments