MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI DON BOSCO YAFANA


Vijana wa skauti kutoka shule ya Sekondari Don Bosco Didia wakimpokea mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) katika mahafali ya 19 ya kidato cha nne mwaka 2017.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akivalishwa skafu na vijana wa skauti.Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo,Padri Mathias Isaka 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza Mkurugenzi wa shule ya sekondari Don Bosco  Didia,Padri Richard Mtui (katikati) na Padri Thomas Kessy 

Kulia ni Padri Thomas Kessy akizungumza jambo wakati viongozi wa shule ya sekondari Don Bosco wakimpokea mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga

Wahitimu wa kidato cha nne wakijiandaa kuingia ukumbini kwa maandamano

Wahitimu wakiingia ukumbini kwa maandamano

Maandamano kuingia ukumbini...

Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiingia ukumbini

Walimu,wazazi na wanafunzi wakiwa wamesimama wakati mgeni rasmi akiingia ukumbini

Wahitimu wakiwa wamekaa ukumbini

Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa ukumbini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa amekaa na viongozi wa shule hiyo

Mkurugenzi wa shule ya sekondari Don Bosco Didia,Padri Richard Mtui akizungumza katika mahafali hayo

Mwanafunzi Jackline Justine akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro,Padri Thomas Kessy na mkuu wa shule Padri Mathias Isaka wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.

Shule ya Sekondari Don Bosco Didia iliyopo katika kata ya Didia wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga leo Jumamosi Novemba 25,2017 imefanya sherehe ya mahafali ya 19 ya kidato cha nne tangu kuanzishwa kwake ambapo jumla ya wanafunzi 141 wamehitimu masomo yao mwaka huu.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mapadri, masisita, walimu, wanafunzi na wazazi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro. 

Akizungumza katika mahafali hayo, Matiro alisema shule ya sekondari Don Bosco Didia ni miongoni mwa shule zenye sifa nzuri kutokana na wanafunzi wake kuwa na maadili mema lakini pia imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali. 

“Hii ni shule inayotufanya Shinyanga tutembee kifua mbele kwa sababu inatoa elimu bora na wanafunzi wanalelewa katika maadili yanayotakiwa hivyo kuwa katika mwenendo mzuri”,alisema. 

Matiro aliwaasa wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha nne kuendelea kuwa waadilifu kwa kufuata mambo mema waliyofundishwa shuleni wanaporudi kwa wazazi wao. 

Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao badala ya kujiingiza masuala ya mapenzi kwani mapenzi na shule haviendi pamoja. 

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa shule hiyo,Padri Richard Mtui aliwataka wahitimu wa kidato cha nne kubeba mazuri waliyojifunza wakiwa shuleni kwa kipindi cha miaka mitano (Pre form one - Form Four)huku akihimiza kumtanguliza mungu katika maisha yao. 

“Nawakumbusha kumtegemea mwenyezi Mungu,dumisheni shukrani kwani shukrani ni hazina ya moyo,tunagemea pia mtakuwa mabalozi wazuri wa shule hii”,aliongeza. 

Naye Mkuu wa shule hiyo,Padri Mathias Isaka alisema elimu waliyoipata wanafunzi hao itawasaidia kuwa mashujaa,wazalendo,kujisimamia kimaadili,kutetea haki,kukemea ukabili na mambo kadha wa kadha ikiwemo kupambana na dawa za kulevya. 

Padri Isaka alisema hivi sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,134 huku akizitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni ukosefu wa bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita. 

0 Comments