Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya ya Kinondoni, Ramadhani Mabula ambaye pia ni Ofisa Taaluma wa Manispaa ya Kinondoni msaada wa madawati na viti 50 kwa Shule ya Sekondari Mikocheni vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5.
Wa kwanza kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mikocheni na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyetabura (wa kwanza kulia) na wageni waalikwa wakishuhudia.
Kutoka kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo, Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya ya Kinondoni, Ramadhani Mabula Ofisa Taaluma wa Manispaa ya Kinondoni, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyetabura na Meneja wa NMB tawi la Mikocheni kwa pamoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa madawati 50 na viti vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Sekondari ya Mikocheni juzi.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyetabura (wa pili kulia) msaada wa madawati na viti 50 kwa Shule ya Sekondari Mikocheni kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kushoto) akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikocheni iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam madawati yaliyotolea na Benki hiyo kusaidia changamoto ya uhaba wa madawati shuleni hapo.
Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati na viti 50 kwa Shule ya Sekondari Mikocheni iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5.
Akikabidhi msaada huo kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya ya Kinondoni, Ramadhani Mabula, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo alisema NMB imeguswa na uhaba wa madawati kwa shule hiyo na imeamua kuchangia kiasi hicho.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya ya Kinondoni, Ramadhani Mabula, ambaye pia ni Ofisa Taaluma wa Manispaa ya Kinondoni alisema msaada huo kwa Sekondari ya Mikocheni umekuja wakati muafaka ambapo shule hiyo inatarajiwa kupokea wanafunzi wapya miezi michache ijayo.
Aliishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono juhudia za Serikali katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo elimu maeneo anuai ya nchi, na kuahidi wataendelea kushirikiana na NMB. Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyetabura akisoma risala ya shule kabla ya kupokea msaada huo, aliishukuru Benki ya NMB kwa utaratibu wa kutumia sehemu ya faida katika shughuli zake kusaidia elimu na aliahidi kuhakikisha msaada waliopokea utatumika ipasavyo ili kuwavutia zaidi wafadhili kuendelea kuisaidia jamii.
"Tunawashukuru sana uongozi wa NMB kwa ujumla kwa kutoa faida katika kampuni yenu na kukumbuka kusaidia jamii. Shule hii ni miongoni mwa shule zilizopata bahati ya kunufaika na mpango wa Benki ya NMB wa kuwezesha kusaidia jamii. Nasi jumuiya ya Mikocheni Sekondari tunawaahidi kutunza viti hivi na kuvitumia kulingana na matarajio ya wafadhili wetu viweze kusaidia wanafunzi..." alisema Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Ndyetabura
0 Comments