SHIRIKA LILILOKOPESHA WANAFUNZI VYUO VIKUU LAJITETEA



SHIRIKA la Maendeleo ya Kijamii nchini (TSSF) limesema kuwa linafanya kazi zake kihalali na kuwa kesho asubuhi litawasilisha nakala za uhalali wake huo kwenye Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako katika Mkutano wa Bunge unaoendelea Dodoma, akimjibu Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi aliyeomba mwongozo kuhusu uhakika wa TSSF katika kutoa mikopo nafuu kwa wanafunzi wa elimu ya juu, alikana kulifahamu na kutaka watu kulipuuza.

Kutokana na kauli hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TSSF, Donati Salla, jana alitoa taarifa akisema kesho ataenda wizarani kujielezea kuhusu uendeshwaji wa shughuli zake hizo akiwa na nakala muhimu za shirika hilo.

Salla alisema hadi jana hakuwa amepewa barua rasmi ya kumtaka kuripoti, lakini hata hivyo alisema kwa sasa shirika lake halina mrejesho wa kusema dhidi ya tamko la Waziri Ndalichako kuhusu yeye na wizara yake kutoitambua TSSF licha ya shirika hilo kufanya jitihada mbalimbali za kujitambulisha kwa wizara

0 Comments