Madarasa ya shule ya msingi ya Tologo ambayo yamejengwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.
Evarist Pascal ambaye ni mchimbaji mdogo akitoa maelezo kwa mkuu wa Wilayaya Geita(ambaye yupo katikati)shughuli za ujenzi na ghalama ambazo zimetumika kujenga madarasa hayo.
Madarasa ya shule ya msingi ya Tologo ambayo yamejengwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.
Diwani wa Kata ya Nyarugusu,Swalehe Juma akielezea na kuonesha darasa ambalo bado halijakamilika.
Wachimbaji wadogo kwenye Kata ya Nyarugusu na Serikali ya kijjiji na kata hiyo wameshirikiana kuchangia ujenzi wa madarasa manne na ofisi 2 za walimu kwenye Shule ya Msingi Tologo iliyoezuliwa na upepo na kubaki darasa moja.
Akizungumza na mkuu wa wilaya ya Geita , wakati alipokwenda kujionea shughuli na jitihada ambazo zinafanywa na wachimbaji wadogo za kuboresha miundo mbinu ya elimu,Bw Evarist Pascal alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa hali ambayo ilisababisha wanafunzi kusomea madarasa ambayo yalikuwa yameezuliwa na mvua walionelea ni vyema wakichangia ujenzi huo hili watoto wapate sehemu nzuri ya kujisomea.
Hata hivyo ameendelea kutaja kuwa ujenzi wa madarasa hayo pamoja na ofisi za walimu umegharimu kiasi cha Sh, Milioni 56.
Aidha ameendelea kusema kuwa kitongoji cha Tologo kinakabiliwa na upungufu wa zahanati ya mama na mtoto kwa kuwa ipo zahanati moja ya Boko ambayo imeelemewa na kwamba ili kuchangia ujenzi huo wametengeneza madirisha 11 na kufyatua matofali elfu 3
Kutokana na juhudi ambazo wamezifanya Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewapongeza wachimbaji hao na ameahidi kushirikiana nao ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.
0 Comments