WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KUANZA MITIHANI YA UPIMAJI

Kwa ufupi

Wanafunzi 521,855 wa kidato cha pili wamesajiliwa kufanya mtihani huo.

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza mitihani ya upimaji wa wanafunzi wa kidato cha pili na darasa la nne.

Akitangaza mtihani huo leo Jumapili Novemba 12,2017 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema mtihani wa kidato cha pili utafanyika kuanzia kesho Novemba 13 hadi 24,2017.

Amesema wanafunzi 521,855 wa kidato cha pili wamesajiliwa kufanya mtihani huo.

Dk Msonde amesema mtihani wa darasa la nne utafanyika kuanzia Novemba 22 hadi 23, 2017 na wanafunzi 1,195,970 wamesajiliwa kufanya mtihani huo.

Amesema maandalizi ya mitihani hiyo yameshakamilika.

0 Comments