Serikali inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa elimu hapa nchini ambao elimu ya msingi itakuwa inatolewa kwa miaka 6, tofauti na ilivyo sasa ambapo hutolewa kwa miaka 7.
Akijibu swali linalohusu watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Joseph Kakunda ametolea ufafanuzi suala hilo na kusema kwamba mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima.
“Napenda kutoa majibu sahihi waliopata mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu huko tunakoelekea inabadilisha mfumo wa sasa wa elimu ambao utahitaji mtoto aanze chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari miaka minne na itakuwa ni lazima”, amesema Mheshimiwa Kakunda.
Mheshimiwa Kakunda ameendelea kwa kueleza kwamba kutokana na mfumo huo mpya ambao utaruhusu mwanafunzi kusoma kwa muda mfupi, na baada ya kuhitimu ndio utakuwa kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na ndipo ataruhusiwa kuolewa.
Hivi karibuni Waziri kakunda alitoa taarifa ikisema kwamba ili mtoto wa kike aweze kuolewa atahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu sekondari, suala ambalo liliibua mjadala kwa wananchi.
0 Comments