Afrika ndio sehemu inayopatikana chuo kikuu kikongwe zaidi, (chenye miaka mingi zaidi) duniani.
Chuo hiko ambacho kimetajwa na UNESCO na Guiness Book of World Records, kinajulikana kama University of Al Quaraouiyine na kipo nchini Morocco, chuo hiko kilianzishwa mwaka 859 ambapo mpaka sasa ni takriban miaka 1159.
Kilianzishwa na Bi. Fatima bint Muhammad Al-Fihriya Al-Qurashiya akishirikiana na Madrasa ya eneo hilo, na kuanza kutoa elimu ya dini ya Kiislam, na mpaka sasa kinaendelea kufanya kazi kwa kutoa elimu ya vitivo mbali mbali vya elimu zote ikiwemo ile ya Dini ya Kiislam na elimu ya dunia kama inavyoitwa na wengi.
#Afrikayetu
0 Comments