Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega amempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) kwa kazi kubwa anayofanya ya kuwaletea wananchi maendeleo hasa katika kuboresha sekta ya Elimu jimboni hapo.
Mh Ulega ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.Kompyuta hizo 22 zenye thamani ya Tsh 44 milioni zimetolewa na Mbunge Mavunde pamoja na wadau wa maendeleo katika kusaidia kuboresha sekta ya Elimu jimboni hapo.
Aidha akitoa maelezo mafupi katika hafla hiyo,Mh Mavunde ameahidi kuzipatia kompyuta shule zote 130 na kuahidi kuboresha miundombinu ya nishati katika shule zote ili wanafunzi wengi zaidi wapate nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia ikiwa ni muendelezo wa ugawaji wa vifaa vya kieletroniki katika mashule ambao ulitanguliwa na ugawaji wa vishkwambi (tablets)500 zenye thamani ya Tsh 1 Bilioni.
Akmkaribisha Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa ameahidi kushirikiana na Mbunge kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.
0 Comments